GET /api/v0.1/hansard/entries/1425317/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1425317,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425317/?format=api",
"text_counter": 254,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Upande wa gavana, Seneta na MP ni kama shule ya msingi na sekondari. Sijawahi kuona mwanafunzi ametoka shule ya sekondari na kurudi shule ya msingi. Kwa hivyo, sio sisi tuliwaambia MPs walio na chuki na kiburi watafute kiti cha Seneta au gavana. Lakkini wakitaka kiti cha Seneta wangoje miaka mitano ijayo . Kuanzia siku ya leo, Wabunge wote 290 wajue kuwa kuna Maseneta 67 na kaunti 47. Tuna uwezo wa kuangalia vile magavana wanafanya kazi katika kaunti zote. Sio vizuri ati Wabunge kusema kwamba pesa ya gavana inaliwa. Kwani wao ni Maseneta? Kwa hivyo, napinga Mswada huu kwa asilimia mia moja kwa sababu ni wa aibu katika Kenya yetu. Hakuna mtu mkubwa kama Seneta. Seneta ni mkubwa kuliko MP akifuatwa na gavana. Asante. Ni mimi Seneta wa Embu County, daktari ambaye ni deputy party leader wa Kenya Kwanza."
}