GET /api/v0.1/hansard/entries/1425345/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1425345,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425345/?format=api",
"text_counter": 282,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kwanza kabisa, Mswada huu ulichapishwa kinyume na Kifungu cha 113 cha Katiba yetu. Kabla ya kuchapishwa, Mswada huu haukupelekwa kwa Spika wa Seneti ili kuuidhinisha kama anakubali kuwa hauathiri kaunti. Hii ni mojawapo ya taratibu ambazo zinazingatiwa na Katiba kuhusiana na Miswada ambayo inapelekwa katika Mabunge yote. Itakumbukwa kwamba mwaka wa 2019, Seneti ilikwenda mahakamani, Mahakama ikabatilisha karibu sheria 25 ambazo zilikuwa zimepitishwa na Bunge la Taifa bila kuletwa katika Seneti. Kwa vile Mswada huu unaathiri Seneti na ulichapishwa, ukajadiliwa na kupitishwa katika Bunge la Taifa bila Spika wa Seneti kuuidhinisha, hiyo ni kinyume na Katiba. Hilo ni jambo la kwanza. Kwa hivyo, lazima tuukatae Mswada huu."
}