GET /api/v0.1/hansard/entries/1425351/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1425351,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425351/?format=api",
    "text_counter": 288,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, ijapokuwa Kanuni zile zilikua zimepitishwa na Bunge la Kitaifa na wakasema walikuwa wamefanya uhusishaji umma kwa upana, lakini hawakuhusisha umma kwa zile gatuzi zimekuwa zikipokea wakimbizi. Kwa mfano, gatuzi za Garissa, Turkana, Mombasa, Busia na kwingineko, hazikuhusishwa kuangalia Mswada huu. Kwa hivyo, ikawa mawazo yaliyotoka pale yalikua kinyume na yale ambayo Bunge la Taifa ilikuwa imepata. Swala hilo la uhusishaji umma tulilijadili juzi katika Kamati hio wakati tulipokua tukiangalia kanuni mpya za Affordable Housing. Swala la uhusishaji umma ni swala la kikatiba na haliwezi kuondolewa na sheria kama hii ambayo tunaizungumzia."
}