GET /api/v0.1/hansard/entries/1425445/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1425445,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425445/?format=api",
    "text_counter": 61,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Kuna sehemu ambazo mababu waliotutangulia walizikwa na mahali walikuwa wanafanyia sherehe za kitamaduni. Maeneo hayo lazima yapewe kipaumbele katika kufidia serikali za kaunti na jamii husika. Pia kuna sehemu za ibada na mbuga za wanyama ambazo vile vile lazima zishughulikiwe. Serikali inapotaka kuwekeza katika kaunti hizo, ni lazima iwape watu hao kipaumbele. Bw. Naibu wa Spika, naomba upeane mwelekeo kwa Waziri husika katika sekta ya maji. Kando na bwawa ambalo tunajadili litanufaisha watu wa Tharaka Nithi na Kitui, kuna mabwawa mengine katika nchi ya Kenya ambayo Serikali ya Kenya Kwanza itaanzisha. Lazima wawajibike na kueleza nchi mikakati ambayo wataweka ili kuhakikisha kwamba hakutakuwa na kulalama kwa watu wa kaunti nyingine kwa Seneti wanapopewa nafasi kutokana na changamoto kama zile ambazo watu wa Tharaka Nithi na Kitui wanapitia. Tharaka Nithi na Kitui ziwe kaunti ambazo zitapeana mwelekeo wa jinsi miradi ya Serikali ya mabwawa ya maji na unyunyizaji mashamba itakavyokuwa inatekelezwa."
}