GET /api/v0.1/hansard/entries/1425556/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1425556,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425556/?format=api",
"text_counter": 172,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa marekebisho ya sheria ya National Construction Authority yaani shirika linalosimamia ujenzi katika nchi yetu ya Kenya. Mabadiliko haya yako wazi na yatasaidia pakubwa kuchangia kina mama, vijana na pia walemavu kupata fursa ya kufanya biashara kama wanakandarasi nchini. Wanawake na vijana ndio asilimia kubwa ya idadi ya watu walioko nchini. Wengi wametengwa katika biashara na makazi kwa sababu uchumi wetu haujakuwa wa nguvu ili kuweza kumchukua kila mmoja. Mswada huu utatoa fursa ya kuwezesha wao kufanya biashara ili waweze kujikimu na pia waajiri watu wengine ambao watafanya kazi katika kampuni ambazo zitakuwa zinafanya kazi ya ujenzi. Sheria ziko, lakini katika utekelezaji wazo utaona mambo mengi yanakwenda kinyumenyume. Kwa mfano, ijapokuwa vijana wana asilimia katika kandarasi zinazotolewa na kaunti zetu utapata wanakandarasi wengi ni watu wa umri mkubwa lakini wanatumia majina ya vijana kama wakurugenzi kwenye kampuni zile ili wapate biashara. Lakini kwa ukweli kampuni sio zao na pesa zinakapokuja vijana wanapewa pesa kidogo kulingana na pesa ambazo zimepatikana. Vile vile wanawake wengi wameshindwa kuingia katika biashara kwa sababu ya ukosefu wa raslimali/ capital. Ijapokuwa kuna taratibu ama Miswada ambayo imeletwa kusaidia, kwa mfano, Hustler Fund, pesa hizi zimekuwa donda sugu na wengi wameshidwa kulipa kwa sababu uchumi ni mbaya na hawawezi kufanya biashara kwani kaunti zetu hazilipi pesa kwa wakati. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}