GET /api/v0.1/hansard/entries/1425557/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1425557,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425557/?format=api",
    "text_counter": 173,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Pia Serikali ya kitaifa hailipi pesa kwa wakati. Kwa hivyo, hata wakifanya biashara zile hawapati malipo ama faida kama vile inatarajiwa katika kufanya biashara hiyo. Wengi ambao wanaanzisha biashara wanapata changamoto nyingi hususan changamoto za raslimali yaani mtaji wa biashara ile. Utapata hata kama amepewa kandarasi, inataka alipie mali ghafi ama vitu ambazo atatumia kwenye ujenzi ama kupeleka kwenye biashara. Hivyo basi wanakosa kufanya biashara hizo kwa sababu ya pesa hizi ama mtaji raslimali inayohitajika kuanzisha biashara hizo. Vile vile Mswada huu unapendekeza kuwa wale ambao fee haizidi shilingi 15,000 waruhusiwe kufanya maombi hayo bila kulipa. Mswada huu utasaidia pakubwa kuimarisha hali ya kina mama, vijana na walemavu katika nchi yetu. Pia utasaidia pakubwa kuinua biashara na kuhakisha kwamba watu wengi wanafanya biashara ambazo zitasaidia kuendeleza maisha yao kuliko kusubiri kuajiriwa. Kazi zimekuwa adimu sana kwa sababu uchumi wetu haukui jinsi unavyopaswa. Kodi mpya zitakazotozwa zitazidi kulemaza biashara katika nchi yetu ya Kenya. Asante, Bw. Naibu wa Spika, kwa kunipa fursa hii."
}