GET /api/v0.1/hansard/entries/1425593/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1425593,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425593/?format=api",
    "text_counter": 209,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Zamani kulikuwa na sheria ambayo ilikuwa inatoa mazao yote kwa jumla; Agriculture and Food Authority (AFA) . Lakini sheria hii ilipatikana kukusanya mazao yote ya biashara na chakula pamoja na ikawa vigumu kupata uangalizi wa kimaada kwa yale mazao mbalimbali. Hivyo ndivyo basi kukakuwa na sheria kutoka 2017/2018 ambayo ilikuja na wazo kuwa kila zao liwe na sheria yake. Ndio maana sasa kuna sheria ya kahawa, chai, ukuzaji miwa na sukari. Mazao haya yote yameweka chini ya heria mbalimbali. Hii ni kwa sababu kila zao linatiliwa mkazo kivyake."
}