HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1425603,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425603/?format=api",
"text_counter": 219,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "na pia kujiendeleza kimaisha. Lakini, mtambo ulipofungwa na kuuzwa, mpaka hivi sasa, wakulima wametatizika. Kwa muda wa miaka 10, Serikali ya Kaunti ya Kilifi haikuweza kuekeza pesa kununua mtambo ule ili iwe ni raslimali yao. Kwa hivyo, kaunti zetu hazijawekeza katika mazao haya na ukulima kwa jumla. Ukiangalia bajeti za kaunti ya Lamu, Mombasa, Kwale, Kilifi na Taveta Taita, ni asilimia ndogo sana ambayo tunaekeza katika ukulima. Ilhali, mazao haya yana uwezo ya kuwanasua watu wetu kutoka lindi la umaskini na ukosefu wa pesa. Bw. Spika wa Muda, Kifungu cha 22 cha Mswada huu kinasema kwamba kaunti zitatunga sheria kuhusiana na masuala ya uandikishaji, utumaji maombi na mambo mengine ambayo yamezungumziwa pale. Mswada huu tayari unatoa mwongozo kuhusiana na vile ambavyo kaunti zetu zitaendesha mambo yao. Kwa kuchelea kwa sheria ambazo zitagongana, yaani sheria ya kaunti na ya kitaifa, itakuwa wazo bora kama sehemu hii itarekebishwa au iondolewe kikamilifu. Hii nafasi katika Kifungu cha 38 ambacho kinampa Waziri mhusika kwa masuala ya ukulima, akishirikiana na bodi ambayo imeanzishwa hapa na sheira hii, pamoja na serikali za kaunti ziweze kutengeneza kanuni za kusimamia masuala kama hayo ambayo yanazungumziwa hapo. Kwa mfano, ya uandikishaji na mengineo ambayo yamezungumziwa katika Kifungu cha 22. Jambo lingine la kunifurahisha ni kwamba, bodi itakuwa na makao yake makuu katika sehemu ya Kilifi. Hii iko katika kifungu cha nne. Lazima tutoke katika ile kasumba ya kuweka kila kitu katika jiji la Nairobi. Wakati fulani, tulikuwa tunazungumzia masuala ya uvuvi na ikasemakana kwamba, makao makuu ya shirika la uvuvi yatakuwa South C katika jiji la Nairobi wakati uvuvi ufanyika Mombasa na Ziwa Victoria. Hakuna sababu ya makao makuu ya uvuvi kuwa jijini Nairobi. Kwa hivyo, hili wazo la makao makuu kuwa Kilifi itasaidia pakubwa. Kwa sababu, bodi itakuwa pale pale ikiangalia maslahi ya wakulima, wanunuzi na wale watakuwa wakifanya biashara ya nazi. Masuala mengine ni kwamba, nazi inaweza kusaidia pakubwa kumaliza umaskini katika pwani. Lakini, tumeona kwa muda sasa, minazi ambayo inazaa ni ile babu zetu walipanda. Hatujafanya jambo lolote ambalo litaweza kusaidia kuhifadhi zao la mnazi na korosho katika hii miaka ambayo tumeishi sisi, takriban miaka 30. Bw. Spika wa Muda, ni muhimu kwamba kaunti zetu ziweze kufanya utafiti wa mazao yetu. Wapewe vitega hamu vya kuhakikisha kwamba haya mazao ya kimila ya pwani yakuzwe kwa wingi ili yalete faida kwa watu wetu. Tukiangalia zao la korosho, hakuna kinachopotea. Korosho ikiwa iko juu, yale makanju yanaweza kutengeneza juice nzuri sana. Ukiangalia zao la nazi, likiwa ni dafu, unaweza kunya madafu. Inasaidia kusafisha system yako ya urine na kuhakikisha kwamba unaisha na afya. Nyama iliyo katika dafu, inasaidia pia kuinua platelets za mgojwa. Huu ni utafiti uliofanywa kitambo na majeshi ya kule sehemu za Indonesia na kwengineko. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}