GET /api/v0.1/hansard/entries/1425604/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1425604,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425604/?format=api",
    "text_counter": 220,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Nazi nazi yenyewe inaweza pikwa, kukaushwa na ikafanywa mafuta. Hata kama siwezi kwenda katika kiwanda kikubwa, viwanda vidogo vya kukamua mafuta vinaweza kuchangia pakubwa kuinua hali ya nazi na maisha ya watu wa pwani. Kama alivyosema Sen. Hamida; hupotezi chochote kwa nazi kwa sababu makuti inaweza kutumika kufunika paa la nyumba yako. Hata kama kuna joto, huwezi kuihisi ukiwa na paa la makuti. Unaweza kupata kamba kutoka kwa makumbi ya nazi. Pia unaweza kutengeneza godoro kutoka kwa zao ya nazi. Nazi ina faida nyingi sana kwa watu wetu. Kwa hivyo, sheria hii itasaidia pakubwa. Pia naona majukumu ya kaunti zetu yamezungumziwa kwa undani kabisa katika Kifungu cha 21 ya sheria hii. Sheria hii itawaleta pamoja wakulima wa mazao haya. Kwa mfano; wakulima wa korosho na nazi watawekwa katika vikundi vya cooperatives ili waweze kupata mikopo kwa njia rahisi na kufundishwa mbinu mpya za ukulima ili waweze kujikimu kimaisha. Ukisafiri kutoka Kilifi kwenda Malindi, utapata watoto wengi wanauza korosho ambazo zimetayarishwa kienyeji. Hiyo ina maana kwamba, iwapo wazo hili litapata soko, watu wengi watapa njia za kukimu maisha yao ili waweze kusomesha watoto wao na kupata ruzuku ya kuwawezesha kimaisha. Kwa hivyo, naunga mkono sheria hii isipokuwa Kifungu cha 22. Kinapswa kiangaliwe tena kwa sababu kina nafasi ya kutatiza majukumu ya kaunti zetu ambazo zimezungumziwa katika Kifungu cha 21 na vile vile katika Kifungu cha 38 cha Mswada huu. Haya mazao mengine yote kama vile castor beans, cashew nut oil seed ya ingaliwe. Mafuta mengi yanayotumika hapa Kenya yanaagizwa kutoka Malaysia na Indonesia. Halafu baadaye, yanakuwa processed na kuuzwa hapa nchini. Kuna nafasi ya kukweza sun flower, jojoba na palm oil inayomea katika maeneno ya pwani na kwengineko. Hii yote ni mimea inayoweza kumea pwani ili watu wetu wapate ajira na tuweze kupata viwanda vidogo vidogo. Bw. Spika wa Muda, katika ruwaza ya Serikali ya Kenya Kwanza, wamesema kwamba watafanya zile zinaitwa aggregated industrial parks . Viwanda kama hivi vidogo vidogo ndio vinaweza kuhudumu, kusafisha bidhaa kama hizi na kuziuza nje ili nchi yetu ipate fedha za kigeni. Bw. Spika wa Muda, nakubaliana na Sen. Hamida kwamba haya mazao yaliyozungumziwa hapa yanafanya vizuri pia katika sehemu ambazo ni kame. Sehemu kama vile Embu ambapo pana ukavu kidogo panaweza kupandwa simsim. Vile vile, katika kaunti ya Tharaka-Nithi, Makueni na Kitui. Ni mimea ambayo inaweza kufanya vizuri katika maeneo ambayo hayana maji mengi. Kwa hivyo, ni zao ambalo linaweza kusaidia pakubwa kuinua nchi yetu kiukulima. Vile vile itatusaidia kuanzisha viwanda vidogo vidogo. Viwanda hivi ni kama ngazi ya kuwezesha sisi kuwa na viwanda vikubwa ambavyo tutavihitaji hapa nchini ili tuweze kuendelea. Bw. Spika wa Muda, asante kwa kunipa fursa hii."
}