GET /api/v0.1/hansard/entries/1425606/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1425606,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425606/?format=api",
    "text_counter": 222,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, asante kwa kunipa fursa kuchangia Mswada ambao umeletwa Seneti na Seneta Hamida. Mimi ni Naibu wa Mwenyeketi katika kamati ya kilimo. Tuko na furaha kwa sababu nakumbuka wiki jana tulitembea Mombasa na wiki zijazo tutakuwa Kirinyaga, Meru, Kaunti yangu ya Embu na kaunti zingine kule Rift Valley. Huu ni Mswada ambao unaweza kusaidia mambo ya kilimo. Katika ile manifesto ya Serikali ya Kenya Kwanza, mambo ya kilimo yamezingatiwa sana na ndio maana pesa ya kilimo imekuwa ikiongezeka. Tuko na uhakika kwamba katika Bajeti ya mwaka ujao wa Serikali, mambo ya kilimo hapa nchini yatatengewa pesa nyingi. Tunajuwa kilimo ni pesa mfukoni. Inasaidia kwa sababu kilimo kinafanywa na watu wote, vijana kwa wazee, walioajiriwa na wasioajiriwa. Naunga mkono kwa sababu tunataka pia Serikali Kuu iweze kuongezea pesa ili kuwe na walimu wa kufunza watu kilimo cha kisasa katika kaunti zote 47. Kilimo cha zamani kilikuwa kwamba ukipanda miti au mimea mingine inakawia kuwa tayari. Kuhusu kilimo ya makadamia, Kaunti ya Embu ina sub-county nne. Watu wengi pale Manyatta na Runyenjes Sub-county upande wa juu ya Embu wamepanda zao hili. Tunafurahi sana kuunga mkono Mswada wowote ili mkulima awe na furaha miaka yote. Nakumbuka wakati tulipochaguliwa tulikuta kwamba makadamia kutoka Kaunti ya Embu iligharimu shilingi 30 kwa kilo moja. Tulipopiga kelele nikiwa mmoja wao, kilo moja ya makadamia kwa sasa ni shilingi130. Kama Seneti, tunaweza kusaidia kwa kuunga mkono miswada itakayosaidia mkulima. Serikali ya Kenya Kwanza nayo ihakikishe imetoa pesa za mbegu na walimu wa kusaidia watu kupanda mimea isiyochukuwa muda mrefu kukomaa. Kaunti nyingi zimekubali kulima. Wabunge nao waongezee mgao wa bajeti kwa kilimo. Tutakapofanya kazi hiyo yote ya macadamia, nazi na njugu ambazo Seneta Hamida ametaja itakuwa vizuri ikiwa Serikali ya Kenya Kwanza itatutafutia soko nchini Marekani, Dubai na nchi zingine ili mkulima apate kujifurahisha kupata pesa ya karo, hospitali na kadhalika. Pia naunga mkono kuwa na vyama vya ushirika vitakavyomsaidia mkulima. Kwa sababu mambo ya kilimo ni shughuli ya serikali za kaunti, inafaa magavana na wakulima waketi pamoja ili kilimo kiboreshwe mashinani. Kaunti zingine huwa semi-arid kama vile Mbeere North na Mbeere South katika Kaunti ya Embu. Wapelekewe wale watu wanaojua mambo ya mchanga upimwe vizuri ili zile kaunti ziweze kupanda mimea kama iliyotajwa. Hakutawezekana ikiwa wale watu kama agricultural officers hawako. Ningeomba Waziri wa Kilimo kwamba kuwe na waterpan na pia dam kubwa. Kwa mfano katika Kaunti ya Embu, sehemu kubwa haina maji. Sehemu kubwa ya Mbeere South na Mbeere North haina maji ya kutosha. Tuweze kupata dam kama ile tumeahidiwa na Serikali ya Kenya Kwanza ili sehemu hizo ziwe na kilimo bora. Sio mambo ya makadamia pekee. Kuna cash crops kama miraa na nyingine. Nahakikishia Serikali kuwa ikiwa itafanya kazi hiyo yote, ushuru utaongezeka na haitaenda kukomba na kukopa pesa huko nje. Serikali za kaunti vilevile zitapungungiwa na mzigo wa kukosa fedha. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}