GET /api/v0.1/hansard/entries/1425618/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1425618,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425618/?format=api",
"text_counter": 234,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Githuku",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13595,
"legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
"slug": "kamau-joseph-githuku"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa fursa hii ili niweze kuchangia Mswada huu muhimu ambao unahusisha ukuzaji wa korosho na nazi. Nashukuru Sen. Kibwana kwa kuleta Mswada huu kwa wakati unaofaa. Tulikuwa tunahitaji Mswada huu sisi kama wakaazi wa Pwani. Nazi na korosho ni vitega uchumi katika kanda yote ya Pwani. Mswada huu utasaidia kufanikisha wakulima wetu ili wapate kitega uchumi ambacho kinazingatiwa kisheria. Wakulima wa Pwani waweze kuuza mali yao. Ili kusaidia wakulima wetu, Serikali, kupitia Wizara ya Kilimo na Mifugo, lazima ifanye utafiti mwafaka kuhakikisha wanapata mbegu nzuri za uzalishaji wa korosho na nazi. Hiyo ikizingatiwa vizuri, tutaweza kuimarisha uchumi wa wakazi wa kaunti za Pwani na kwingineko katika Jamhuri yetu ya Kenya ambako mimea hiyo inakuzwa. Natoka katika Kaunti ya Lamu ambayo ni mojawapo ya kaunti ambazo zinaweza kutoa mazao mazuri ya korosho. Kuna Kisiwa cha Faza kule Lamu Mashariki. Ni mahali ambapo panakuzwa korosho nzuri sana. Zimefanyiwa utafiti na zimeibuka kuwa bora zaidi. Ni korosho ambazo zinaweza hata kupelekwa katika nchi za nje na kuuzwa katika mataifa ya kigeni ili kuimarisha uchumi wa wakazi wa Kaunti ya Lamu. Ni muhimu sana Serikali, kupitia Wizara ya Kilimo na Mifugo kuona kwamba dawa ambazo zinatumika kunyunyizia mimea hiyo zinapatikana. Wakati mwingine unakuta kwamba mimea hiyo inavamiwa na wadudu na kuathiri mazao. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}