GET /api/v0.1/hansard/entries/1425619/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1425619,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425619/?format=api",
"text_counter": 235,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Githuku",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13595,
"legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
"slug": "kamau-joseph-githuku"
},
"content": "Ni vyema Wizara ya Kilimo na Mifugo ifanye utafiti. Wanafaa kutoa dawa mwafaka ambazo zitasaidia. Dawa hizo zisiwe na madharau ya moja kwa moja kwa mkulima na mazingira. Hilo likifanyika, bila shaka mazao yatapatikana kwa wingi na kusaidia wakazi wa sehemu mbalimbali. Pia naunga mkono kwamba tutafute masoko katika nchi za nje ili wakulima wetu watie bidii kwa sababu mazao hayo yanahitajika. Serikali ikiwahakikishia kwamba wanapokuza mazao hayo watapata masoko katika nchi za nje. Ikifanya hivyo, bila shaka itasaidia sana wananchi wetu na Kenya nzima. Bw. Spika wa Muda, kuna jambo ambalo limekuwa likiendelea. Watu kutoka nchi za nje wamekuwa wakija kununua mazao hayo. Wananyanyasa wananchi kwa kununua kwa bei ya chini. Ni vyema tuwe na taratibu kwa mambo ya bei ili wakati mazao hayo yanapelekwa kuuzwa katika nchi za nje, bei inayofaa imewekwa kuwasaidia wakulima wetu ili waweze kujinufaisha kiuchumi. Zao lingine ambalo linajulikana zaidi katika mwambao wa Pwani ni nazi. Nazi ni kitegauchumi kikubwa cha wakazi wa Pwani, kuanzia Mombasa, Kilifi na Lamu. Ni zao ambalo limekuwa likisaidia sana watu hao. Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Mswada huu ambao umeletwa na Sen. Kibwana kwa sababu utahakikisha kwamba wananchi wote wanafaidika kutokana na Serikali kuweka taratibu za kuuza mazao yao. Naomba tuupitishe kama Seneti ili kusaidia wananchi ambao tumekuja hapa kuwakilisha. Huu ni Mswada ambao umekuja kwa wakati mwafaka. Ni Mswada ambao utasaidia wananchi wetu waweze kujiimarisha na kujiendeleza kiuchumi, ikizingatiwa kwamba kuna taratibu kwenye mazao mengine kama vile miwa na makadamia za kusaidia wakulima. Hili ni zao ambalo halikuwa na taratibu lakini sasa ni wakati mwafaka. Wananchi wetu watapata fursa ya kusaidiwa. Vile vile, watahisi kwamba walishughulikiwa na kuzingatiwa na Seneti. Asante, Bw. Spika wa Muda. Naunga mkono Mswada huu."
}