GET /api/v0.1/hansard/entries/1425683/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1425683,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425683/?format=api",
"text_counter": 37,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mithika Linturi",
"speaker_title": "The Cabinet Secretary for Agriculture and Livestock Development",
"speaker": {
"id": 69,
"legal_name": "Franklin Mithika Linturi",
"slug": "franklin-linturi"
},
"content": "Sen. (Dr.) Murango amenitia katika kona ambayo nawezashindwa kujieleza vizuri. Naomba niweze kujaribu kumjibu. Ningependa kusema na ieleweke vyema kwamba kazi tunayofanya, hasa tunafuata ajenda ya Bottom-Up Economic Transformation Agenda (BETA) . Tunataka kuongeza mauzo ya nje ya nchi kwa majani chai, kahawa, maziwa na kadhalika. Nahakikishia Seneti hii kwamba tuko na nia ya kuhakikisha kahawa inayotoka katika nchi yetu inaendelea kuongezeka kila wakati. Tutaendelea kuuza kahawa kwa kuwa tunauza hata sasa. Compliance na regulations ni kuhakikisha hatukosi soko. Ndio sababu tunajitahidi kufuatilia sheria hizi ili kuhakikisha soko yetu au kahawa tunayopeleka kule haina tatizo lolote. Nilikuja Jumatatu asubuhi kutoka nje ya nchi nilipokuwa pia natafuta soko ya bidhaa za Kenya. Nataka kuwahakikishia ya kwamba siyo tu kule EU peke yake, tayari tumepata njia ya kupeleka majani chai na kahawa kule Uchina. Wakati nilipokuwa huko tarehe 15, nilifungua Trade Centre ya bidhaa ya Kenya na wale wakulima tuliokuwa nao. Tumeweka hata sahihi na mikakati ya kuhakikisha ya kwamba kahawa na chai yetu inaweza kufika kwa soko zile zingine. Kile ningetaka kusema ni kuwa Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha ya kwamba, tunaweza kusukuma soko ya bidhaa zetu tunayokuza hapa ili zifike kule nje. Tunasema lazima tuangalie vile tutaweza kuwa na brand ya kahawa yetu na majani chai iliyo na uhalisi. Kwa sababu ya ubora, kahawa na majani chai isiweze kupotea ili tuwe na brand ambayo inajulikana. Ukienda kule nje, unajua ile kahawa unakunywa inatoka Kenya. Hivyo basi, tutaweza kuhakisha ile kahawa ambayo iko na thamana zaidi kutoka nchi yetu, itaweza kueleweka na kujulikana, ili kuhakikisha tumehifadhi soko yetu. Asante, Bw. Naibu Spika."
}