GET /api/v0.1/hansard/entries/1425687/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1425687,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425687/?format=api",
"text_counter": 41,
"type": "speech",
"speaker_name": "`Sen. (Dr) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Swali la mwisho, Bw. Waziri. Tunajua kwamba katika soko ya kahawa katika mnada wa kahawa Narobi National Coffee Board (NCB) umekuwa ukiendelea kwa muda. Kulingana na stakabadhi na nakala ambazo tumepata, bidhaa hii imekuwa ikiuzwa kwa bei nzuri sana. Ningependa kukuuliza kama unajua ya kwamba wakulima bado hawajaweza kulipwa pesa zao ambazo ni za mazao ya kahawa.Na kutoka jadi, haijawahi kuchelewa ama kufika mwezi wa Mei kama hawajalipwa. Jana nimekuwa na swali ngumu sana kujibu kwa bishop wangu wa kanisa la Anglikana, ambaye ni mkulima. Hata ikambidi asome katika kitabu kitakatifu cha Biblia kuona kama kazi ya mkulima ni kuteseka bila malipo. Ningetaka niulize kama kuna kufuatilia kwokwote kunafanyika katika vyama vya ushirika, kuhakisha ya kwamba wakulima wamelipwa kabla mwezi huu kuisha, kwa sababu ukweli ni kwamba kahawa imeuzwa na pesa zipo. Ni vizuri walipwe ili waweze kunufaika na dola kwa sababu waliuza dola ikiwa juu. Na vile inaendelea mambo huenda yakaharibika zaidi. Kwa hivyo, swali langu ni hilo. Je, unajua ya kwamba wakulima wa kahawa hawajalipwa na kahawa imeuzwa? Je, wataweza kulipwa kabla mwezi huu haujaisha?"
}