GET /api/v0.1/hansard/entries/1425694/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1425694,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425694/?format=api",
"text_counter": 48,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mithika Linturi",
"speaker_title": "The Cabinet Secretary for Agriculture and Livestock Development",
"speaker": {
"id": 69,
"legal_name": "Franklin Mithika Linturi",
"slug": "franklin-linturi"
},
"content": ", NationalTreasury and Economic Planning na Wizara yangu tumetengeneza memo ya kuweza kuvutilia mbali madeni yote katika cooperatives na inayodaiwa wakulima wa kahawa. Tumeweka kidole na tutavutilia mbali madeni waliyo nayo ili wakulima wa kahawa waweze kufaidika na waweze kuendelea kukuza kahawa. Kwa hivyo, Sen. (Dr.) Murango, hayo ndiyo tunayoyafanya. Kujua kama kweli ni pesa ngapi ama wakulima hawajalipwa na kama watalipwa kabla ya mwezi wa tano kumalizika, ningeomba unipee nafasi niwasiliane na ndugu yangu, Chelugui, kwa sababu hiyo ndiyo Wizara yake ya uuzaji wa kahawa na kulipa wakulima. Kazi yangu ni kuzalisha. Nikimaliza kuzalisha na kupeleka kwa factory na ichukuliwe na cooperatives, kazi yangu huishia hapo. Mambo ya uuzaji na ulipishaji sasa hushughulikiwa na Wizara ya Co-operatives and Micro, Small and Medium EnterprisesDevelopment . Bw. Naibu Spika, yale ninayoeleza ni yale ninayoyajua na tunafanya kazi pamoja. Nitamfikia rafiki na ndugu yangu Waziri ili nijue ni wakati gani watakaolipa na pale juhudi za malipo zimefika. Ikiwezekana, tutakutumia jibu kwako binafsi na pia hapa Bungeni. Nikisema watalipwa kesho ama kesho kutwa na hii ni kazi ya Wizara nyingine, nitakuwa na uhakika. Sitaki kusema mambo nisiyo na uhakika nayo katika Bunge hili."
}