GET /api/v0.1/hansard/entries/1425707/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1425707,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425707/?format=api",
    "text_counter": 61,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika kwa nafasi hii. Namkaribisha Waziri wa Kilimo baada ya mchakato mgumu kuhusu pembejeo. Langu ni kuuliza Mhe. Waziri swali moja au mawili. Eneo la Magharibi, hasa Kaunti ya Bungoma, kuna upanzi wa kahawa. Juzi kumekuwa na madai na ishara kwamba kuna ulanguzi wa kahawa kutoka viwanda vya usagaji kahawa katika Kaunti ya Bungoma kuelekea nchi jirani. Pia, gharama ya ukuzaji wa kahawa katika nchi jirani ya Uganda ni bora zaidi kuliko nchi ya Kenya. Vile vile, wakulima wanadai kwamba mfumo wa malipo wa fedha za kahawa hauwapi motisha na nishati ya kufanya ukulima. Hivi kwamba, karibu wakulima waanze kukata miti ya kahawa na kujiunga na taasisi ama ukulima mwingine. Mwisho kabisa ni kwamba, katika upanzi na biashara ya kahawa halmashauri ya viwanda kule Bungoma kuna madai ya ubadhirifu wa fedha za wakulima katika taasisi hizo. Ni mikakati ipi ambayo imewekwa na Serikali na Wizara yako kuhakikisha"
}