GET /api/v0.1/hansard/entries/1425716/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1425716,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425716/?format=api",
    "text_counter": 70,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika, nilikuwa na maswali mawili, lakini nitauliza moja. Nitafuata maagizo yako. Ningependa kuuliza Waziri wa Kilimo swali moja kama Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Mimi hufurahia kwani kilimo kwenye Serikali ya Kenya Kwanza ni pesa mfukoni. Jana ilikuwa ni maadhimisho ya siku ya majani chai ulimwenguni. Kahawa na majani chai haina tofauti. Wakulima wengi hulima upande moja wa shamba majani chai na upande mwingine kahawa. Pia leo ni siku ya kusherehekea. Kenya ni namba tatu ulimwenguni kwa panzi wa majani chai. Bei ya chai imerudi chini. Bw. Waziri, uwasaidie wakulima wa majani chai ili wapate faida kubwa. Serikali ya Kenya Kwanza inapendekeza tax irudi chini ndio mkulima asherehekee. Utafanya nini ili dunia nzima ikisherekea, bei ya majani chai iwe inayofaa ili mkulima aweze kulipa karo ya watoto wake shuleni, alipe pesa za hospitali na kusimamia familia yake. Wakulima wameumia na kulia. Nauliza swali hili kama mkaazi wa Embu. Kaunti ya Embu ni moja ya kaunti ambazo zinalima majani chai. Ukulima huu unafanyika katika eneo la Manyatta Runyenjes. Ukulima wa majani chai unafanyika Kirinyaga, Rift Valley na Kaunti ya Meru."
}