GET /api/v0.1/hansard/entries/1425812/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1425812,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1425812/?format=api",
"text_counter": 166,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Cherarkey",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13217,
"legal_name": "Cherarkey K Samson",
"slug": "cherarkey-k-samson"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, nashukuru Waziri wa Kilimo kwa kupata fursa kufika katika Bunge la Seneti. Nashukuru kwa yale mabadiliko anafanya kwenye sekta ya kilimo ingawa najua siyo sekta rahisi. Ningependa kuuliza Waziri atoe hakikisho kwa taifa – tumeona kwenye vyombo vya habari kwamba kuna upungufu wa pembejeo ambayo inawekwa juu ya mahindi. Kwa lugha ya Kimombo ni top dressing. Anaweza hakikishia wananchi kuwa kuna pembejeo ya kutosha katika maghala ya kitaifa kwa wakulima wa mahindi. Mwisho, ametenga ridhaa kwa wale wakulima ambao walipata matatizo ama shida wakati wakupata mbolea mwezi uliopita. Bw. Waziri alikuwa Kaunti ya Nandi jana na alisema kutokana na ile subsidy inatolewa ya mbolea tumepata mapato zaidi, hasa sekta ya majani chai. Waziri atoe hakikisho kwa wakulima wa Kenya. Na aseme neno moja tu na roho zetu kama wakulima wa taifa la Kenya zitatulia."
}