GET /api/v0.1/hansard/entries/1426006/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1426006,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1426006/?format=api",
"text_counter": 67,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa nafasi hii. Ningependa kuendelea na mchakato wa majidiliano kuhusiana na fedha za dharura na changamoto za dharura zinazokumba nchi hii. Ni jambo la muhimu Seneti, kando na kuzungumza kila uchao kuhusiana na utepetevu wa serikali za kaunti kupambana na majanga haya, lazima tumulike matumizi ya fedha zilizowekwa katika bajeti za kaunti tunazotoka. Maeneo mbalimbali hupata majanga ya moto. Kufumba na kufumbua, kabla ya wawekezaji kuzima moto huu, moto huwa umechoma kila kitu. Unapata magari ya wazimamoto yanakuja baadaye, masaa 12 baada ya janga kuharibu mali ya umma. Bw. Naibu Spika, ukifuata vitabu vya hesabu unapata kuna fedha zinatumika kudhibiti hali hizi. Naomba uamrishe viongozi wenzangu wawe na nidhamu katika jumba."
}