GET /api/v0.1/hansard/entries/1426014/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1426014,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1426014/?format=api",
"text_counter": 75,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Bw. Naibu wa Spika, inaashiria kuwa Seneta alikuwa anasinzia nilipokuwa natoa hoja zangu. Ndio mkoko unaalika maua. Mafuriko nchini humu yameathiri familia nyingi. Jana jioni kwenye Wadi ya Chesikaki katika Eneo Bunge la Mlima Elgon, kulikuwa na maporomoko ya ardhi ambayo yalifunika watu wanne wa jamii moja. Mmoja alipata majeruhi makubwa sana. Tunaeleza athari za mafuriko. Lazima serikali za kaunti ziwajibike katika matumizi ya fedha ambazo tunapeleka mashinani. Tunataka zionekane kuwa zinafanya kazi. Isiwe kwamba ni fedha ambazo zinatumika kufurahisha na kufanya viongozi kuishi maisha ya starehe. Kuanzia sasa, naomba sisi kama Seneti tuweze---"
}