GET /api/v0.1/hansard/entries/1426522/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1426522,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1426522/?format=api",
"text_counter": 224,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Ningependa nichukue muda mfupi sana kama dakika mbili na moja itakayosalia nimzawadi Sen. Mandago ili aweze kutaja jambo moja au mawili. Kwa kifupi, shilingi 400 bilioni sio pesa kidogo. Mara nyingi tunapouliza maswali magavana, wengine hupandwa na hasira na jazba na kupinga maseneta kufuatilia jinsi fedha hizi zinavyofanya kazi. Ni lazima wajue sasa hivi wanatusikiliza pamoja na watu katika kaunti ambazo tunatoka, Biblia inasema kwamba iwapo umepewa vingi, ni lazima uwajibikaji uwe wa hali juu. Tunajitolea mhanga tokea sasa kuhakikisha ya kwamba wanawajibika kwa fedha tunazowapa. Ni lazima mabilioni haya yawape vijana wetu kazi. Pia walemavu na wamawake wapewe kazi na iweze kuonekana katika vitabu vya hesabu. Pesa tunazileta mashinani. Kwa hivyo, ni lazima wanakandarasi na wanabiashara walipwe pesa zao kwa wakati unaositahili. Madeni ambayo tunayaona kila uchao, ni lazima yalipwe ili kaunti zetu ziweze kuonekana zinafanya kazi kwa mujibu wa Katiba. Juzi, tumeona katika uchambuzi wa Mdhibiti wa Bajeti akisema kuwa baadhi ya magavana wako na akaunti nyingi katika benki zisizoeleweka na hazijulikani zinafanya nini. Ni lazima wawajibike. Asante, Bw. Spika, na ninamkaribisha Sen. Mandago kwa dakika moja aweze kutaja mambo mawili kwa wananchi wa Kenya."
}