GET /api/v0.1/hansard/entries/1426530/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1426530,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1426530/?format=api",
"text_counter": 232,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chute",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13583,
"legal_name": "Chute Mohamed Said",
"slug": "chute-mohamed-said"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Nachukua fursa hii kushukuru kamati ambayo pia mimi ni mwanakamati kwa kufanya kazi nzuri sana. Tulitumia masaa mengi kukubaliana na upande huo mwengine wa National Assembly kuhakikisha kwamba kaunti zinapata pesa zinazohitajika. Tulikuwa na Kshs385 bilioni miaka iliyopita. Kama kamati, tulikaa masaa mengi na baadaye, tukakubaliana pesa ambazo pia Serikali inaweza kusaidia kaunti, ni Kshs400.1 bilioni. Ni vizuri kaunti zijue kwamba Seneti inaunga mkono ugatuzi. Tunataka kaunti zipate pesa zinazohitajika ili maendeleo yafanyike. Shida tuko nayo ni kwamba kaunti zingine zina shida ya kutumia pesa inavyotakikana. Maendeleo iko katika asilimia sita na 10. Kulingana na vile ambavyo Seneti inatafuta hizo pesa, tungependa sana kaunti zichunge pesa na maendeleo isikuwe chini ya asilimia 30. Bw. Spika, kwa mfano, kaunti kama Marsabit, tuko na shida kubwa. Pesa inafujwa na Seneta akiuliza, gavana anatuma watu kwa redio kwenda kusema kwamba kabila lake linakuwa targeted . Nilikuwa nasema kaunti za Waisilamu lakini Sen. Abass akanikataza--- Wanaharibu pesa na kuumiza raia ambao wanastahili kupata huduma katika kaunti hizo. Ningetaka Mhe. Kindiki achunguze mambo ambayo yanaendelea katika Kaunti ya Marsabit. Gavana wa Marsabit anatuma wazee kwa redio waseme kwamba kabila fulani inakuwa targeted . Hadi unashangaa vile sisi hukaa kwa masaa mengi kutafuta pesa ili kaunti zipate pesa na ikifika huko, wanagawa katikati ya familia na marafiki."
}