GET /api/v0.1/hansard/entries/1426661/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1426661,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1426661/?format=api",
"text_counter": 363,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Naunga mkono Mswada unaozungumzia mambo ya IEBC. Ningeomba haya mambo yaangaliwe kwa njia inayofaa. Wale makamishna tisa tutakaowakubali waangalie mipaka ya maeneo Bunge inavyofaa. Nakumbuka wakati tulichaguliwa, kulikuwa na shida ya malipo kwa wale waliopatiwa kandarasi ya magari ya kubeba watu waliokuwa wanasimamia kura. Mpaka wa leo, watu wa kaunti nyingi hawakupata zile pesa. Nakumbuka tulikaa kama mwaka mmoja hadi wakati niliposoma taarifa hapa, ndipo watu wengine wakalipwa. Haya mambo yanafaa yaangaliwe na njia inayofaa. Tuliletwa hapa na wananchi na tumekubaliana kwamba mambo mengi yaende hadi mashinani. Serikali ya Kenya Kwanza inasema mambo ya kilimo na afya, yaende mashinani kwa mwananchi. Ndio maana siku hizi tunazungumzia mambo ya ugatuzi. Mambo mengi yanaangaliwa na Wabunge wa Bunge la Kitaifa lakini watu wanaojua mambo ya kaunti ni magavana na maseneta. Hii ni kwa sababu baadhi ya mambo kama mashamba yamegatuliwa kwa kaunti zetu. Bi. Spika wa Muda, ningeomba mambo ya mipaka yaaangaliwe, Kaunti ya Embu tuko na constituency nne. Hakuna hata moja inafaa kuguswa. Zibaki hizo constituency nne na Wabunge wanne na Seneta mmoja, women representative na gavana mmoja. Hii ni kwa sababu tukichukua mkondo mwengine tutaanzisha vita na haitakuwa vizuri. Ningeomba wadi ziongezwe kwa sababu tuko na wadi chache. Kwa mfano, Mbeere North Ward iko na wadi tatu. Kuna moja inaitwa Evurore Ward ambayo ni kubwa. Inatoshana na wadi mbili kwa pamoja. Kama itawezekana, hiyo wadi igawanywe ziwe wadi mbili. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}