GET /api/v0.1/hansard/entries/1426662/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1426662,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1426662/?format=api",
    "text_counter": 364,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Upande wa Mbeere South, tuko na wadi tano lakini ukiangalia Mavuria Wadi, Mbeti South na Mwea pia nazo ni kubwa. Naomba wale watu watakaongalia haya mambo, wasipunguze wadi. Wanafaa waongeze wadi ziwe nyingi ili mwananchi afaidike. Upande wa Embu North tuko na wadi nyingi. Kuna Nginda, Kirimari na Kithimu wards ambazo ni kubwa na ziko na watu wengi. Ningeomba wadi zingine ziongezwe. Mambo ya kusema watu waunganishwe na wengine haifai. Kuna wadi kama Runyenjes na Gaturi North ambazo ni kubwa sana. Kwa hiyo, ningeomba wadi za Embu zisipunguzwe hata moja. Mambo ya mipaka pia yaangaliwe. Ukiangalia vijiji vya Mbeere North, utakuta kuna watu wako upande wa Kaunti ya Tharaka Nithi. Wakati wa kura wanapiga kura vizuri lakini kuna mgawanyiko kati ya watu wa Kaunti ya Embu na Tharaka Nithi. Utakuta wanapigania watu kila mmoja akisema watu fulani ni wetu na wale ni wetu. Kwa hiyo, wale watu tutakaochagua waangalie vile mwananchi atafanyiwa kazi inavyofaa. Bi. Spika wa Muda, ningeomba zile constituency nne za Kaunti ya Embu zibaki hivyo. Mbeere South ni kubwa sana. Ningeomba iongezwe ziwe mbili ili tuwe na Wabunge wawili. Katika Embu North, wadi kama Gaturi, Kithimu na Mbeti North, ziunganishwe pamoja ndio tuongezewe constituency nyengine. Naomba ile kamati itakayoshughulikia haya mambo iongeze constituency zingine mbili katika Embu County. Moja itoke Mbeere na nyengine upande wa Embu. Naomba haya mambo yaangaliwe vizuri ili yule mwananchi aliyetuchagua tuje Seneti afurahie. Wakati hayo mambo yatafanyika, itakuwa vizuri kwa sababu mwananchi ataweza kuhudumiwa kwa njia inayofaa. Ndio maana mara nyingi tumepigania ugatuzi ili magavana wapatiwe pesa inayofaa kuenda mashinani. Wakati tutakapoongezewa wadi na constituencies, najua itasaidia national Government kupeleka pesa kule mashinani ndio mwananchi aliyetuleta hapa ahudumiwe inavyofaa kwa upande wa kilimo, afya, elimu na mambo mengine. Bi. Spika wa Muda, naunga mkono lakini mambo mengine yanafaa yaangaliwe. Kama Seneta wa Kaunti ya Embu, katika zile constituencies zetu nne, hakuna hata moja inafaa iguswe. Naunga mkono kuwa tuongezewe zengine mbili na pia wadi ziongezwe, ili tuwe na wadi nyingi ili mwananchi afayiwe kazi vizuri. Kama Seneta wa Kaunti ya Embu, naunga mkono lakini kunafaa kuwe na marekebisho. Ni mimi Seneta wa Kaunti ya Embu, Sen. Munyi Mundigi, ambaye ni daktari na Deputy Party Leader wa chama cha Democtatic Party (DP). Asante."
}