GET /api/v0.1/hansard/entries/1426801/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1426801,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1426801/?format=api",
    "text_counter": 92,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante Bw. Naibu Spika. Cha kwanza, naunga mkono Mswada huu ambao unahusu mageuzi ya Tume huru ya kusimamia kura na mipaka katika Kenya. Cha muhimu ni kuwa Mswada huu ulitengenezwa na Kamati ya NADCO na hatimaye, ikaletwa katika Bunge. Tulisikizana ya kwamba, ikitoka katika Bunge la Kitaifa, wataileta katika Bunge la Seneti ili iweze kujadiliwa na kukubaliana. Kwa mda mrefu sana, hii nchi yetu ya Kenya imeketi bila kuwa na Tume ya kusimamia mambo ya kura. Ni jambo la kusikitisha sana kwa sababu hakuna nchi ambayo inaweza kuwa haina tume huru ya kusimamia mambo ya kura. Kwa hivyo, naunga sana mkono Mswada huu kwa sababu uko na mambo mengi ambayo yanaweza kusaidia upigaji kura. Kitu cha kwanza ambacho mimi naunga mkono zaidi ni kwamba, inaleta mwelekeo. Tukizingatia ya kwamba katika nchi yetu ya Kenya, tunaendelea kuwa na wingi wa watu. Vile vile, itahitaji kuona ya kwamba katika wingi wa watu, kuna mageuzi kidogo baada ya mda, ili kuona ya kwamba majina, mipaka na maeneo bunge, yameangaliwa na kugeuzwa. Katika mwelekeo, tunaangalia wingi wa watu ili tuweze kujua ni wadi ngapi zinawezwa kuongezwa katika maeneno fulani, ama maeneo bunge mangapi yanaweza kuongezwa kulingana na vile watu wanavyozaana katika nchi yetu. Pia nataka kuunga mkono Mswada huu kwa sababu unanuia kuangalia kina nani wanafaa kuteuliwa kama Wabunge. Mswada huu unapendekeza kuwe na watu wawili watakaoteuliwa na Parliamentary Service Commission (PSC). Mmoja wa watu hao atatoka katika party ya walio wengi na mwingine katika party ya walio wachache. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}