GET /api/v0.1/hansard/entries/1426806/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1426806,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1426806/?format=api",
    "text_counter": 97,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunisahihisha. Mmoja atatoka chama cha walio wengi na mwingine atatoka chama cha walio wachache. Pia Mswada huu unapendekeza Law Society of Kenya (LSK) kuteua mtu mmoja. Vile vile, kutakuwa na mtu mmoja kutoka Institute of Certified Public Accountants of Kenya (ICPAK). Pia kuna watu wawili watakaoteuliwa na Inter- Religious Council of Kenya (IRCS). Mapendekezo ya kamati ya NADCO yamejumuishwa na sasa tuna Mswada kutoka Bunge la Taifa. Kulingana nami, hii ni sheria ambayo itatoa mwelekeo mzuri katika nchi yetu. Pia Mswada unapendekeza kuteuliwa kwa katibu atakayesimamia jopo hili. Katibu huyo atafanya kazi kwa kandarasi ya miaka minne. Haifai kuwa miaka mitano. Hapo kuna suitofahamu kuwa atakuwa na kandarasi ya miaka minne ilhali tunafanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano. Tunahitaji maelezo mwafaka kwa nini mtu huyo awe na kandarasi ya miaka minne badala ya mitano. Bw. Naibu Spika, mwisho ni kwamba Mswada huu unazingatia mambo ya kupiga kura na matakwa yanayohitajika kisheria. Kwa hivyo, naunga mkono."
}