GET /api/v0.1/hansard/entries/1426883/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1426883,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1426883/?format=api",
"text_counter": 174,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Kwa hiyo, tukipata watu wenye tajiriba kuu ambao wanaweza kusimamia haki, itakuwa bora kwa nchi yetu kwa sababu, tutaweka matatizo yanayotokea baada ya kura kuisha katika kaburi la sahau. Vilevile, sheria hii itatoa nafasi kwa IEBC kusimamia mipaka ya maeneo bunge na wadi katika nchi yetu. Tumeona kwamba kutoka katiba ipitishwe mwaka wa 2010, hatujaweza kukagua tena maeneo bunge ili kubadilisha majina ama kutoa mipaka mipya ya maeneo yetu. Kumekuwa na mkurupuko wa wingi wa watu katika maeneo yetu. Tunapata kwamba maeneo mengine yana watu wengi kupita kiasi. Sio sawa kwa eneo bunge kuwa na wapigaji kura zaidi ya laki tatu, ilihali maeneo bunge mengine yana wapiga kura elfu ishirini ama thelathini. Hii ni kwa sababu tunataka tuwe na usawa wa uwakilishi katika nchi yetu. Watu hawafai kupata shida kutafuta Mbunge wao kwa sababu ana watu wengi sana wa kuwasimamia. Swala hili la mipaka lazima liende katika Bunge la Kitaifa na pia lije Seneti. Hii ni kwa sababu Seneti ndio inayosimamia ugatuzi ambao unawakilishwa mashinani na bunge za kaunti. Kwa sababu bunge la kaunti linachaguliwa moja kwa moja kutoka kwa wananchi, itafaa kwamba Mswada wa kubadilisha maeneo wadi, lazima yafika katika Seneti ili uangaliwe na kukaguliwa sawasawa. Kwa kumalizia, ni masikitiko kwamba tumeona Bunge la Kitaifa limewatimua makamishna wa zamani bila ya kufuata mwongozo wa kisawasawa. Ile tume iliyochaguliwa na Mhe. Raisi, wao ndio walishitaki, wenye kuchunguza na wao ndio waliotoa hukumu ya kuwaondoa watu wale. Inafaa kwa siku za usoni, Mswada wowote wa kuwaondoa makamishna ufikishwe katika Seneti. Hii ni kwa sababu, wao ndio wanaosimamia kura za magavana, wabunge na maseneta. Kwa hiyo, ni lazima tuwe na uamuzi kwa suala hilo Asante, kwa kunipa fursa hii."
}