GET /api/v0.1/hansard/entries/1427240/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1427240,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1427240/?format=api",
    "text_counter": 318,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, nashukuru kwa kunipa nafasi nami nitoe maoni yangu kuhusu Mswada huu ambao tunaujadili mchana huu. Mswada huu hasa ni juu ya vile kaunti zetu zinaweza kuongeza ushuru katika gatuzi zao kupitia mtambo wa kijitali. Ni maoini ya Kamati ya Bajeti na Fedha kuwa tuwe na sheria ambayo inayosema kila gatuzi nchini Kenya iwe na namna ya kuchukua hela bila kutumia wanadamu ama a computerized system, kwa lugha ya kiingereza. Kila wakati wafanyikazi wa Serikali, iwe ni wa kaunti au Serikali kuu wakiitishwa kubadilisha mambo kutoka kwa mfumo wa kuchukua hela kupitia mwadamu iende kwa mashine ambazo hazijui mwanadamu, huwa wanaipinga sana. Wanapinga kwa sababu wanajua ya kwamba wakati ambapo unaondoa mwanadamu katika ile hali ya kuchukua hela zozote za Serikali, shimo la kuchukua rushwa linazibwa. Kwa hivyo, watu wengi Serikalini kwa nafasi kubwa ama ndogo kwenye sehemu ya kuchukua hela hawapendi tukibalisha namna ya kuchukua hizi pesa kutoka kwa wananchi; badala ya kutumia mwanadamu kuandika risiti, iandikwe na tarakilishi. Lakini, sasa tunataka kuipitisha hii sheria--- Hapa Seneti, tumeona shida kubwa sana. Kwa mfano, kule Tana River, hadi leo hawajaweka automated system ya kukusanya pesa za kodi zinazotolewa na wananchi ili kufanya kazi ya serikali ya kaunti hiyo. Watu wanaofanya kazi katika kaunti yetu wamekataa kabisa. Sababu moja wanayotoa ni kwamba automated system ni bei ghali sana. Katika Kaunti ya Tana River, pesa zinazofujwa kupitia njia hiyo ya kukusanya ushuru bila kutumia mashine ni nyingi sana. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}