GET /api/v0.1/hansard/entries/1427243/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1427243,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1427243/?format=api",
    "text_counter": 321,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "unayopewa ili kulipa, kwa mfano, ada ya soko ya Tana North Sub-County, ni tofauti na ile ya Tana Delta Sub-County. Baada ya pesa hiyo yote kuwekwa kwenye hizo paybill numbers inachukuliwa na mwanadamu ambaye ni Director for Revenue . Kule Tana River, nambari kadha wa kadha zinatumika kama paybill . Zikifika idadi fulani, nambari hizo zinadhibitiwa na Directorfor Revenue katika kaunti yetu. Yeye ndiye huchukua pesa hiyo na kuipeleka kwa akaunti ya kaunti inayojulikana kama County Revenue Fund (CRF) Account. Pesa hizo zinalipwa kutumia paybill kisha mwanadamu mwingine huenda na kuzitoa ili kuweka kwa akaunti. Kwenye harakati hizo, kuna shimo kubwa ambapo pesa za wananchi wa Tana River zinafujwa. Hakuna namna ambayo kodi au ada ambazo zimetozwa na risiti kuandikwa zinakaguliwa kuthibitisha usahihi wa pesa inayowekwa kwa akaunti. Shimo hilo limefanya watu ambao wanafanya katika Idara ya Kukusanya Ushuru katika Kaunti ya Tana River kuwa matajiri. Utapata kuwa mtu ni tajiri ilhali hana kampuni au shamba lakini amejenga nyumba nyingi. Wanahepa kujenga kule Tana River na kwenda kujenga Malindi, Mombasa na Nairobi. Hii ni sheria ambayo tukipitisha katika Seneti itasaidia kufichua wizi unaofanyika katika kaunti zetu. Siyo Tana River pekee. Watu wengi wanajua kwamba risiti zinaandikwa lakini pesa zinazolipwa hazifiki kwenye CRF Account . Kwa mfano, kule kwetu, watu wanapewa paybill numbers ambazo hazilinganishwi na rekodi. Hujui kama pesa unayolipa itakwenda kwa akaunti au la. Ukimaliza kulipa, stori yako inaishia hapo. Ni watu wanaotumia hizi systems kuiba usiku na mchana. Katika Kaunti ya Tana River, Gavana alianzisha Inuka Fund . Hizi zilikuwa ni pesa ambazo watu wetu walikuwa wanaomba ili wajiinue kibiashara. Halafu shida ikatokea kwamba, watu hawarejeshi pesa walizoomba. Halafu, sasa kuna mtu ameanza kusema tuwapatie Paybill Numbers . Hiyo ni sawa na ile wanayofanya huku kwa County Revenue Fund (CRF). Wanataka tena ku introduce"
}