GET /api/v0.1/hansard/entries/1427246/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1427246,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1427246/?format=api",
"text_counter": 324,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kila wakati, watu wanasema eti tukitafuta mtambo au utomated system ni ghali. Lakini, ukiangalia zile pesa ambazo zimeibwa tangu Kaunti ya Tana River ianze mpaka leo, hata afadhali tutumie mamilioni lakini tununue system, japo hawataki kufanya hivyo. Ukiangalia Magavana ambao wamekuwa hapo, hakuna hata mmoja ambaye ameisukuma hii system . Swali tunalouliza ni kwa nini hawataki kufanya automatedsystem ya revenue collection . Sababu ni kwamba, hapa katikati, kuna mashimo. Haya mashimo wanajua ya kwamba hizi pesa zinafaidi maafisa na sio watu wa Tana River. Ndio maana watu wengi wanapigania kuwa Revenue Collection Officers. Wanataka hiyo kazi. Kazi hii ni sawa na ile ya polisi wa trafiki. Sababu ni kwamba kuna kitu watu wanachofanya. Mpaka leo, hilo shimo halijafungwa. Kila kaunti hapa Kenya imeachiwa kuchagua vile itakusanya kodi kwa kaunti. Ukija Nairobi wako na system yao, Mombasa wako na system yao pia. Pia kaunti zingine ziko na system zao. Kaunti yetu haina system . Ni vile tu babu zetu wa Tana River County Council walikuwa wanakusanya kwa kuandika risiti za uwongo. Hiyo ndio"
}