GET /api/v0.1/hansard/entries/1427248/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1427248,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1427248/?format=api",
"text_counter": 326,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "inayotumika mpaka sasa. Mswada ambao umeletwa leo tuujadili kwa makini kwa sababu ukiwa sheria italeta usawazishaji wa ukusanyaji wa kodi katika kaunti zetu zote. Kaunti zote za Kenya zitakuwa zinatakikana kutumia automated system za Revenue collection tutakapopitisha Mswada. Kila pesa tunayokusanya ili kufanya kazi ya wananchi itaenda kwa akaunti ya CRF ambayo kwa sasa haiko. Kwa hivyo, mimi nasimama hapa kwa niaba ya watu wa Tana River kusema ya kwamba tunataka sana kuupitisha Mswada huu. Sheria hii italeta uwazi na tutajua wale wezi. Tukipitisha Mswada huu kuna watu watajiuzuru kazi kule Tana River na kwingineko. Kwa sababu wamekuwa wakiiba pesa kupitia hii system ambayo haifanyi kazi. System ya zamani ambayo haiko automated na haina kompyuta. Ni aibu kufanya kazi na kupata mshahara lakini unakula pesa kidogo inayotoka kwa wananchi na wanakosa maendeleo. Kaunti ya Tana River ni Kaunti ya tatu ama pili au mwisho kwa kukusanya ushuru wa moja kwa moja ilhali watu wetu wanalipa ushuru. Maseneta wote wapitishe Mswada huu ili magavana ambao hawafanyi haki kwa wananchi na kuficha siri za pesa wanazozichukua kutoka kwa wananchi waanikwe mbele ya Wakenya wote. Wizi mkubwa unaendelea na magavana wanajua kuwa katika County Revenue"
}