GET /api/v0.1/hansard/entries/1427251/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1427251,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1427251/?format=api",
    "text_counter": 329,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Magavana na mawaziri wa kaunti inafaa washurutishwe kupitia kwa Mswada huu kuweka automated System. Pili, waweze kuhimizwa kwamba baada ya mwezi wanatoa ripoti ya pesa ambazo wamekusanya. Hili jambo litapunguza wizi. Yeyote atakayetaka kuiba lazima ahusishe wote waliochaguliwa kwenye Bunge ya Gatuzi. Nafahamu kuwa kuna waliochaguliwa kwenye county Assembly na wana roho ya kusaidia wananchi. Hawakuingia kwenye bunge kuiba na kujitajirisha. Bw. Spika wa Muda, huu ni Mswada mzuri na inafaa tuupitishe. Hasa kwa sababu ya kaunti zetu ambazo zinaongozwa na watu ambao hawana moyo wa kusaidia wananchi. Mwananchi anapeleka ng’ombe zake kwa soko ambayo ushuru unachukuliwa. Lakini soko kama ile ya Bangale ambayo ndio kubwa na inakusanya pesa nyingi katika Kaunti ya Tana River, hakuna choo kilichojengwa. Serikali ya kaunti inachukua pesa kila siku katika soko hiyo. Soko ya Garsen haina facilities kusaidia mwananchi wa kawaida kufanya kazi yake na wananchi wanalipa ushuru. Mwisho wa mwaka, Kaunti ya Tana River inaandikwa kama Kaunti ya pili kutoka mwisho kwa kukusanya pesa za Own Source Revenue. Hii ni kwa sababu hakuna sheria ambayo inafaa. Hii ndio sheria ya kwanza ambayo tunasawazisha kaunti zote ili wizi unaoendelea na utajiri wa udhalimu uishe. Ndio maana wengine wanakuwa wagonjwa. Unaona tajiri ambaye anasafiri kutafuta matibabu. Hakuna raha katika nyumba yake kwa sababu pesa ambazo amesomesha watoto wake ni pesa za wizi. Pia watoto wanakuwa wezi na wanafyatuliwa risasi. Pia Watoto wanakuwa drug addicts kwa sababu walisomeshwa na pesa za wizi. Hakuna baraka katika nyumba hizo. Wao wanakaa na kufa kwa magonjwa mabaya kwa sababu walikula pesa za uwizi za Tana River. Walisomesha watoto wao na pesa za uwizi na udhalimu. Ninasema hii sheria itasaidia sana kaunti zetu na italeta uwazi katika matumizi ya pesa. Ikiwa kila mwezi kuna ripoti ambayo itawasilishwa mbele ya County Assembly, watajua kama kuna pesa zinazofunjwa. Ikiwa kila mwezi kuna ripoti inakuja hapa Seneti, tutajua kwamba kuna pesa zinaibwa ama zinatumika njia mbaya. Bw. Spika wa Muda, mimi nimefurahi sana. Kama kuna Mswada mmoja ambao tumeupitisha kwa Bunge la Seneti ambao utasaidia wananchi na watajua ukweli wa mambo ambao unaendelea kule nyumbani, basi ni Mswada huu tunaoujadili sasa. Tunasema na kuchukua nafasi hii katika hii Seneti kuwaambia wale jamaa ambao wanafikiria kwa sababu wako kwa kaunti ambazo ziko mbali, kwamba watafanya vile watakavyofanya na watahongana kwa vitengo vya kiserikali ati wasishikwe na kufanya mbinu washike wale majamaa ili wawape mkataba, sisi hapa Seneti tunawaangalia kwa macho mawili. Katika kiingereza tunasema ‘ there is no limitation for criminal liability ’. Yaani ikiwa wewe umeiba au umefanya makosa, hata ukitoka hizo nafasi zako ambazo umeshikilia saa hii, hata kama ni miaka kumi, tukichukua ule ushahidi na tukikuweka pale, wewe utakuwa ni mzee na unataka kustaafu, tutakushika na tutakufunga wakati huo. Tunataka kuwaambia wafanyikazi wa Serikali, sisi hatutaki tena miaka ile ya kusema pande ile tutafanya vile tutakavyofanya, halafu sisi tutaishi kama wakubwa kwa sababu ya pesa. Wewe kama unataka kufanya kazi ya kutafuta pesa, kwa nini usiende kufungua kiwanda au kufanya biashara? Kwa nini unaingia kwa Serikali? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}