GET /api/v0.1/hansard/entries/1427341/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1427341,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1427341/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Olekina",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 407,
"legal_name": "Ledama Olekina",
"slug": "ledama-olekina"
},
"content": "Bw. Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii kwa niaba ya Mhe. Faki ili niombe taarifa kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Elimu. Nimesimama kuambatana na Kanuni ya Kudumu ya 53 (1) kuomba taarifa kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Elimu kuhusu malipo ya malimbikizo kwa walimu waliostaafu kutoka Tume ya Kuajiri Walinu (TSC). Katika taarifa hiyo, kamati: (1) Ichunguze sababu za walimu waliostaafu kutopokea pensheni pamoja na malimbikizo yao ya kustaafu kuanzia mwaka wa 2020 hadi sasa. (2) Iarifu Seneti hii lini walimu hao waliostaafu wataanza kupokea hayo malipo yao. (3) Ieleze pia sababu za Hazina ya Malipo ya Uzeeni (NSSF) kukosa kuwalipa walimu waliostaafu malipo yao ya kustaafu kwa wakati unaofaa. Taarifa hii imeombwa na Sen. Faki, Seneta wa Kaunti wa Mombasa. Asante."
}