GET /api/v0.1/hansard/entries/1435833/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1435833,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1435833/?format=api",
    "text_counter": 99,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika, naunga mkono Mswada wa kuongeza kaunti pesa. Kuna kaunti 47 nchini na nashukuru Maseneta waliozungumza na Wabunge wa Bunge la Taifa. Pesa zilizotengwa kwa magatuzi zimeongezwa kutoka mwaka jana na shilingi bilioni 15. Mwaka wa fedha unaoisha Kaunti ya Embu ilipata Shilingi billion 5.3. Kwanzia mwezi wa saba mwaka huu, Kaunti ya Embu itapokea Shilingi bilioni 5.4. Mswada huu ukipita tutakuwa tumeongezea Kaunti ya Embu Shilingi milioni 200. Pesa hizi hazitoshi lakini naunga mkono. Naomba gavana wa Kaunti ya Embu aangalie ushuru anaotoza kwenye kaunti ili aongeze pesa hizi. Kuna fedha zingine zinatarajiwa kutoka nje kama msaada ili tupunguze madeni kwenye kaunti. Kaunti ya Embu iko na wage bill ambayo iko juu. Pia pending bills ziko juu. Kaunti ya Embu itasaidika wakati gavana atafanya kazi vizuri na Members of County Assembly (MCAs) ili pesa itoshee mahitaji ya Kaunti ya Embu. Gavana wa Kaunti ya Embu inafaa atilie mkazo sekta za kilimo, afya na ujenzi wa barabara. Mazao ya wakulima wa kaunti isiwe na shida ili economy ya kaunti ya Embu ibadilike. Hapo mbeleni tulikuwa na shida lakini sasa naomba gavana afanye kazi ambayo inafaa. Kaunti ya Embu imeteseka kwa miaka kumi lakini kwa miaka tano ya gavana aliyechaguliwa tumeanza kuona mabadiliko. Naomba gavana ajikakamue kwa miaka iliyobaki, ili kaunti iwe kwenye mstari wa kwanza. Miaka itakayokuja tunataka economy ya Embu ibadilike. Ningependa kusisitiza kuwa, miaka inayokuja isiwe ni wabunge wa Bunge la Kitaifa wanatuamurisha vile tunafaa kufanya kazi. Wabunge hawa wanafaa waelewe kuwa kazi ya Maseneta ni kuangalia vile magavana wanafanya kazi. Hii si kazi yao. Naunga mkono. Asante, Bw. Spika."
}