GET /api/v0.1/hansard/entries/1435916/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1435916,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1435916/?format=api",
"text_counter": 182,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante Bw. Spika. Ningetaka kujiunga na wenzangu kuunga mkono Mswada ulio mbele yetu siku ya leo. Ninafurahi kusema kwamba, nikiangalia pesa ambazo zinaenda kwenye Kaunti ya Kirinyaga, ambako mimi ni Seneta, iko na nyongeza kubwa sana katika mwaka huu. Ninaona ya kwamba katika mgao wa kawaida wako na zaidi ya Shilingi bilioni tano na katika conditional grants wako na Shilingi 36 milioni. Tukiangalia mwaka uliopita ambapo walipata Shilingi 5.4 bilioni, saa hii ninaona watapata Shilingi 6.8 bilioni. Katika nyongeza ya pesa ya mwaka huu, ningetaka kuona hospitali ambazo kwa muda hazijamilizwa kujengwa, zikijengwa. Ningependa kuona zahananti za Kiandieri, Kiaritha Nguka, Ngatho; zote zikifanya kazi kwa sababu watu wetu wanaumia. Ningetaka kuona miundo msingi. Ningetaka kuona daraja kama zile za Kibukuria ambazo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}