GET /api/v0.1/hansard/entries/1435917/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1435917,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1435917/?format=api",
    "text_counter": 183,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "zilijengwa na county kwa mbao zikiwekwa chuma ili watoto wetu wawe na usalama wakati wanapovuka, kuenda na kurudi kutoka shuleni. Ningependa kuona madawa katika hospitali zetu. Ningependa ninapo uliza swali nijibiwe kama Seneta kwa sababu saa hii tuko pamoja wakati tunapotafuta pesa lakini wakati tunapopeleka pesa mashinani huwa tunachukuliwa kama tingatinga ambazo zinajenga barabara; ujenzi ukikamilika zinabebwa ili zisiharibu barabara hizo. Ningependa wanakandarasi wale ambao walifanya kazi katika Kaunti ya Kirinyaga na hawajalipwa, waweze kulipwa pesa zao. Pia, ningependa kuona pesa za bursary ambazo zinapewa wanafunzi wetu zimeongezeka ili waweze kwenda shule. Bw. Spika, kazi kubwa ya Seneta ni hii tunayoifanya siku ya leo; kuangalia kwamba kaunti zinapata pesa zao. Sisi ni kama baba ambaye anarudisha mkate katika kaunti ili watoto waweze kupikiwa wale. Nauliza magavana wote wa Kenya mzima kupika pesa tulizoleta na wahakikishe kwamba zimefikia wale wananchi tunoawatumikia. Inaweza kuwa sitapeana bursary au sitafanya maendeleo moja kwa moja, lakini, tumehusika pakubwa kuhakikisha kwamba pesa zimefikia wananchi. Asante Bw. Spika."
}