GET /api/v0.1/hansard/entries/1437214/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1437214,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1437214/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa fursa hii ambayo umenipa kuchangia Mswada wa The County Allocation of Revenue Bill (Senate Bills No.25 of 2024). Kaunti zetu zitapata takriban Shilingi bilioni 401. Hata hivyo, haikuwa rahisi bila kupigana kwa sababu Bunge la Taifa lilitaka kaunti zipate Shilingi bilioni 391. Ilibidi tuwe na Kamati ya Maridhiano. Kuna sababu kadhaa ambazo Wabunge hao walitoa kwa kukataa kupitisha Shilingi bilioni 415 ambazo zilipendekezwa na Seneti. Ya kwanza ni kwa sababu ya ufisadi katika magatuzi. Ufisadi pia uko katika Serikali ya Kitaifa jinsi ulivyo katika serikali za magatuzi. Ni muhimu taasisi husika zipigane na ufisadi katika Serikali ya Kitaifa na zile za magatuzi. Sababu ya pili waliyotoa ni kwamba hawaelewi majukumu ya magatuzi na ndio maana walikataa kupitisha Shilingi bilioni 415. Hilo ni jambo la kushangaza sana kwamba Wabunge wanaopewa kazi ama jukumu la kupeana pesa hawaelewi majukumu ya magatuzi. Labda Wabunge wetu wanahitaji kosi za kuelewa magatuzi yanafanya kazi gani. Nashukuru sana Maseneta kwa kukubali kwamba kazi yetu ni kuhakikisha kuwa pesa zaidi zinaenda katika magatuzi yetu. Wakati magatuzi yanapopata pesa, ni vyema sisi kama Seneti tufuatilie na kuhakikisha kuwa majukumu yaliyogatuliwa yanafanywa jinsi inavyotakikana. Mimi ni Mwanakamati wa Kamati ya Elimu inayoongozwa na Sen. Joe Nyutu. Tunapozuru kaunti mbalimbali, wakati mwingine tunapata kwamba zimewacha jukumu yaliyogatuliwa na kuingilia majukumu ambayo hayajagatuliwa. Ukiangalia bajeti za idara za elimu, utapata kuwa magavana wengi wanatenga pesa za bursaries kwa wanafunzi wa shule za sekondari, vyuo vikuu na Technical, Industrial, Vocational, and Entrepreneurship Training (TIVET). Simaanishi kuwa ni vibaya lakini pia tusisahau majukumu yaliyogatuliwa. Haya ni pamoja na shule za chekechea na vyuo anuwai---"
}