GET /api/v0.1/hansard/entries/1437291/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1437291,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1437291/?format=api",
    "text_counter": 168,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Boy",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13200,
        "legal_name": "Issa Juma Boy",
        "slug": "issa-juma-boy"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika, kwa kunipa fursa niweze kuchangia huu Mswada. Leo nina furaha sana kwa sababu nyanjani watu wengi huuliza kazi yetu ni gani. Leo ndio kazi ya Seneta itatambulika katika nchi hii ya Kenya. Leo Maseneta wamefanya kazi na tumeongeza pesa katika kaunti zetu. Pili, katika mashinani wananchi wengi watukufu wa nchi yetu huuliza mbona Seneta haijengi barabara, shule wala kutoa bursary ? Kazi kubwa ya Seneta ni kuhakikisha kwamba kaunti yake inapata pesa na miradi yote inaendelea vizuri. Bw. Spika naunga mkono Mswada huu kwa sababu kaunti yangu ya Kwale imeongezwa mgao wake na kupata zaidi ya Shilingi 400 milioni."
}