GET /api/v0.1/hansard/entries/1438890/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1438890,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1438890/?format=api",
"text_counter": 200,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Mhe. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Gavana wa Nyeri alivyoongea ako na makosa. Ugavi wa rasilimali unafaa uwe sawa katika taifa zima. Angetaka kumtetea Naibu wa Rais, asingetumia matamshi yale, kwa sababu yanazidi kuleta sitofahamu. Wale walikuwa na haki kupewa fidia ili kuwawezesha kuregesha ule mtambo wa miwa. Lakini kwa yote, tulipomuona kwa ndege ya abiria ya kawaida bila hata walinzi, inatatiza picha ya taifa la Kenya. Nimeona hata Wabunge katika mikutano wakizungumza na kurusha cheche za maneno. Wakenya wakati huu wana matatizo mengi: bei ya bidhaa imepanda. Wakati huu, tunafaa kuongelelea Finance Bill, lakini tetesi ambazo zinakuja katika taifa hili sio nzuri. Ni vipi Naibu wa Rais anatembea na mkoba mkononi? Kama kuna tatizo, inafaa walio kwenye mrengo wa Kenya Kwanza wajaribu kuutatua. Sisi tushazoea matatizo yetu. Tulipigwa, mkatucheka, na sasa kimewaramba. Lakini yote tisa, mkae chini na muyatatue matatizo yenu. Hata leo, mkimshika Spika wa Bunge Hili, ingawaje yuko kwenye mrengo wa Kenya Kwanza, nikiona mtu anamletea shida na anaenda kupokonywa haki zake za kimsingi, nitasimama na kuzungumza yaliyo kweli. Hii ni kwa sababu leo ni yeye, kesho ni mwingine. Tumeona kumetokea tetesi katika Ofisi ya Rais Mstaafu. Mambo haya yanafaa tukae chini, kila mmoja apate haki yake na tuangalie maslahi ya Wakenya. Asante."
}