GET /api/v0.1/hansard/entries/1439448/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1439448,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1439448/?format=api",
    "text_counter": 758,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "tumetamaushwa sana kuona Ksh2.5 bilioni imepunguzwa kwenye ile mipango ya kuwalisha wanafunzi. Mbona pesa zipunguzwe kwenye mipango muhimu kama hiyo ya lishe ya watoto? Kuna vipindi vinavyotendeka kwenye mitandao mbalimbali nchini. Kuna makadirio katika Bajeti ambayo yametengewa ofisi ya Naibu wa Rais na maofisi kadha wa kadha, lakini yale mambo tunayoyaona yanastaajabisha. Kwa mfano, yale makadirio yaliyowekewa Ofisi ya Rais mstaafu, hayakuwafikia. Wasimamizi wa hiyo ofisi wamejitokeza wazi na kusema kuwa hawajapata hata peni licha ya kutengewa fedha kwenye Bajeti iliyopita. Hawana pesa za kuwekea magari yao mafuta wala ya kuendesha ofisi zao. Ninawasihi wahusika wahakikishe kuwa pesa zinapotengwa, ziwafikie walengwa. Siyo haki walimu watatizike kupata marupurupu yao. Hata tumeona viwanja vya ndege nchini viko kwenye hali duni ilhali kila mwaka vimetengewa asilimia fulani ya pesa. Inamaanisha kuwa kuna mfuko umetoboka mahali unaoramba hizi pesa. Kwa yale mambo tumeyazumgumzia awali ya Equalization Fund, miaka nane baada ya kuzinduliwa kwa hazina hiyo, Kaunti za Garissa na Wajir ziko pale pale kimaendeleo na watu wanateseka licha ya pesa kukadiriwa. Hamna stima, maji, na hosipitali ilhali kwenye Bajeti kuu, walitengewa pesa. Kuna uwezekano mkubwa kuwa hizi pesa hazielekezwi kwa walengwa. Kuna mtu mahali anayeifanya makatafunio. Ikiwa tutaekeza Bajeti, ifikie walengwa ili mgao ukija, nifahamu kuwa Kaunti za Wajir, Garissa, Kwale na Mombasa ziko sawa. Ni aibu sana kumuona Naibu wa Rais akizunguka na mabegi kwenye ndege za abiria wa kawaida ijapo ofisi yake iko na bajeti yake. Ni aibu kuyaona hayo mambo yakitendeka kwa wakati huu; ninawasihi wahusika wakuu kuwa Bajeti inapotengwa, iwafikie wahusika. Asante."
}