GET /api/v0.1/hansard/entries/1439938/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1439938,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1439938/?format=api",
    "text_counter": 154,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. ZamZam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": "kipengee cha kuweza kuwalinda watoto wetu, kutakuwa na mwanya. Mtu yeyote kutoka sehemu yoyote ataweza kuchukua mtoto kwa jina la adoption na pengine wanaenda kutumika kwa njia zingine. Hasa, kipengee kile kimelinda mtoto kwa kusema kuwa mwanamume asiweze kuchukua mtoto. Mwanamume hajapewa nguvu ya kulea mtoto kama vile mama. Ningependa hiki kipengee kisiguzwe, ili watoto wetu waweze kupata ulinzi na wasijipate katika mikono ya watu ambao sio wazuri. Watu wengi wanaingia na jina la adoption lakini mwishowe, wanaenda kutumia watoto au kutoa viungo vya mwili. Huwezi kujua kama mtoto anakaa vizuri kwa kuwa hakuna anayefuatilia kule mtoto alipoenda. Ni vizuri mtu wa karibu na wa damu ya mtoto ndio aweze kuchukua mtoto. Naonelea hiki kipengee kisibadilishwe. Asante sana Mhe. Spika."
}