GET /api/v0.1/hansard/entries/1440357/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1440357,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1440357/?format=api",
"text_counter": 182,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "Sisi tunataka uongozi wa mwanamke lakini, uongozi wa mwanamke una matatizo mengi sana. Ni lazima mtoto wa kike apate elimu ya kutosha ili afike kiwango cha kuingia uongozini. Wakati mwingi utapata kuwa mtoto wa kiume anayemtia mtoto wa kike ujauzito huendelea na masomo yake ilhali wa kike anabaki nyumbani. Nimewapa watoto wale nafasi mwaka huu. Watoto waliomaliza Kidato cha Nne ni 21. Nina wengine walio Kidato cha Kwanza hadi cha Tatu na wanaendelea vizuri. Wengine wameungama. Hata walikuwa wameingilia madawa ya kulevya kwa sababu ya stress. Wengi wanashindwa kuamua waangalie mtoto au warudi shule kusoma ili baadaye wapate kazi. Kwa hivyo, wengi wamekwama."
}