GET /api/v0.1/hansard/entries/144037/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 144037,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/144037/?format=api",
"text_counter": 858,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister of State for Special Programmes",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika, Wakenya wana matatizo mengi. Mhe. Kaimu Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha, aliposoma Bajeti yake hivi majuzi, alisema pesa nyingi zipelekwe mashinani. Ninaunga mkono Hoja hii, ili tuweze kwenda kuungana na watu wetu. Itakuwa vyema kama tutawaelimisha jinsi ya kutumia pesa hizo huko mashinani. Kuna pesa nyingi ambazo zimetolewa na Serikali kupitia kwa mpango wa Kazi kwa Vijana. Wakati huu utatufaa sisi sana kama tutashirikiana na wafanyakazi wa Serikali, ili tutumie pesa hizi vizuri. Pesa hizi zimetolewa kwa kupitia Wizara nyingi kama vile Wizara inayohusika na maswala ya vijana, Maji, Barabara na Wizara ya Misitu na Wanyama wa Porini. Ningewasihi waheshimiwa Wabunge wezangu kutumia wiki hizi tatu kuwaelimisha vijana wetu. Huu ni wakati mzuri wa kuwahimiza vijana wetu kujiunga na mpango huu, ili wapate riziki zao."
}