GET /api/v0.1/hansard/entries/144038/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 144038,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/144038/?format=api",
    "text_counter": 859,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Shaban",
    "speaker_title": "The Minister of State for Special Programmes",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, kuna matatizo mengi hapa nchini. Kwa mfano, tumekuwa na upungufu mkuuwa wa mvua hapa nchini. Mimea mingi mashambani imeharibika ingali mibichi. Kwa hivyo, ni vizuri waheshimiwa Wabunge watumie pesa za maeneo Bungeni (CDF) kwa njia ambazo zitawasaidia wananchi wetu. Itakuwa heri ikiwa tutatumia pesa hizo tukishirikiana na Serikali kuanzisha miradi ya kunyunyunyizia mashamba yetu maji. Jambo hili si rahisi kwa Serikali. Ni lazima sisi Wabunge na Serikali kufanya kazi pamoja, ili tuwawezeshe wananchi wetu kupata chakula. Tunaweza pia kutengeneza madimbwi madogo madogo ya maji ili wakulima waweze kupata maji. Tatizo lingine ni kuhusu ugonjwa wa kipindupindu kwa sababu watu wengi hawana maji safi ya kunywa. Ni wakati kama huu tutawaelimisha watu wetu kutumia maji safi."
}