GET /api/v0.1/hansard/entries/144053/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 144053,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/144053/?format=api",
"text_counter": 874,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Nakushukuru, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii, ili niweze kuchangia Hoja hii muhimu sana. Tunajitayarisha kwenda likizo ili kukutana na wananchi na kufanya kazi ya nchi. Wakati wa kipindi hiki, kumekuwa na masuala magumu sana ambayo yameturudisha nyuma kwa maendeleo fulani kwa sababu ya mivutano katika Serikali ya Muungano. Lakini ni maombi yangu na matumaini kwamba vile siku zinaenda, tutaelewa kwamba tuko hapa kwa maslahi ya nchi nzima. Naomba wenzangu hapa kwamba tutakapoenda nyumbani na kukutana na wananchi, tutumie nafasi hii kujenga nchi yetu ya Kenya kwa kuifanya nchi moja. Tuzungumzie zaidi juu ya maovu ya ukabila, ili amani ipatikane katika nchi yetu. Tunaongea mambo ya usalama wa nchi. Kuna ndugu zangu hapa ambao wanatoka sehemu mbali mbali katika nchi yetu na sehemu nyingi sana ambapo wananchi hawana usalama. Ninataka kutoa mwito kwa wenzangu, hasa wale ambao wanatoka sehemu zilizoathiriwa waweze kwenda na kutua ujumbe. Inatishia na kushangaza kwamba ukiona sehemu zinazosemekana kuna vikundi ambavyo vinahatarisha usalama wa nchi. Wakati nchi nzima inazungumza, wale ambao wanahusika, haswa viongozi, hawazungumzii mambo haya; wananyamaza. Halafu, tukija hapa Bungeni, tunamkashifu Waziri wa Mikoa na Usalama wa Nchi."
}