GET /api/v0.1/hansard/entries/144054/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 144054,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/144054/?format=api",
    "text_counter": 875,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, ni jambo la maana sana kuelewa kwamba ili usalama upatikane, lazima sisi sote tutii sheria. Na kama hatutii sheria, itakuwa vigumu sana kudumisha usalama. Kwa hivyo, tunawaomba wananchi, pahali popote walipo, mbali na kuwalaumu polisi – hawa ni watu wetu na ni vijana wetu; hao ni watoto wetu tuliowazaa na mtu habadiliki kuwa Mkenya kwa sababu amejiunga na kikosi cha polisi. Mtu habadiliki kuwa Mkenya kwa sababu amekuwa askari, lakini anabaki kuwa mwananchi wa Kenya. Ndio sababu tunasema kwamba ili usalama upatikane, lazima sisi, kama wananchi, tutii sheria. Bw. Naibu Spika, hakuna mtu anastahili kwenda kuchukua kodi ya haramu kutoka kwa mwengine kwa sababu amekosa kazi. Kuhusisha ukosefu wa kazi ni shida ya nchi na hakuna mtu hata mmoja anaweza kulaumiwa. Ni lazima tujitoe mhanga kama wananchi, tufanye mambo ambayo yanaweza kuleta kazi katika nchi yetu na kuendeleza uchumi wetu katika pembe zote. Lakini hakuna mtu hata mmoja anayestahili kumuua mwingine au kunyakua mali ya mtu mwingine kwa kisingizio kwamba hana kazi! Sio Kenya peke yake ambayo ina ukosefu wa kazi. Tumesikia kwamba Marekani na nchi zote zingine katika ulimwengu mzima ziko na matatizo kama haya."
}