GET /api/v0.1/hansard/entries/144056/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 144056,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/144056/?format=api",
"text_counter": 877,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Jambo lingine ambalo ninataka kuzungumzia, Bw. Naibu Spika, ni kuhusu ukame ambao umekumba nchi hii. Sote tuna shida kwa sababu nchi hii imekumbwa na matatizo haya. Serikali imejaribu kusaidia, lakini mbali na kuwa Naibu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha amesoma Bajeti ambayo sote tuliisifu sana na kusema kuwa ni Bajeti ya mwananchi, ningeomba Serikali kufikiria sana namna ya kuwapatia wananchi maji katika nchi hii, ili tuweze kunyunyizia mashamba yetu na kulima vyakula ambavyo vitatufaa. Hela tunazotumia kwa mambo mengine ambayo hayamhusu mwananchi wa kawaida, tunatakiwa tuyapunguze, tuyaangalie na tuone kwamba maslahi tunayoshika ni ya wananchi. Bw. Naibu Spika, nataka kugusia pesa hizi za miradi ya Constituencies"
}