GET /api/v0.1/hansard/entries/1440689/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1440689,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1440689/?format=api",
    "text_counter": 187,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Makueni County, WDM",
    "speaker_title": "Hon. Rose Mumo",
    "speaker": null,
    "content": "Watu wa Makueni wameniambia hawawezi kuukubali Mswada huu. Wakenya wametoka katika janga la korona ambalo lilifanya wengi wafunge biashara zao. Wengine hawana kazi. Maisha ya Wakenya yamekuwa katika hali ya juu sana. Serikali haijaweka mikakati maalum ya kuboresha maisha yao. Tungekuwa katika Nyumba hii tukiongea jinsi tunaweza kuwasaidia Wakenya waboreshe maisha yao. Kuna njia nyingi za serikali kuweza kupata fedha za kuendeleza mikakati yao. Kizungu kingi kimezungumzwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti. Naomba watumie mbinu hizo, wakae chini kama Kamati na waangalie ni jinsi gani wanaweza kuleta fedha bila kumuumiza mwananchi wa kawaida."
}