GET /api/v0.1/hansard/entries/1441126/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1441126,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1441126/?format=api",
"text_counter": 202,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kisauni, ODM",
"speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
"speaker": {
"id": 13383,
"legal_name": "Ali Menza Mbogo",
"slug": "ali-menza-mbogo"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Spika kwa kunipa fursa niweze kuzungumzia Mswada wa Fedha. Nimesimama kupinga Mswada huu. Kama viongozi, tunapaswa kuheshimu malalamishi ya wananchi na kusikiliza vilio vyao. Kuongeza kwa ushuru wa mafuta kutapandisha bei ya kila bidhaa inayohusiana na mafuta. Jambo hili halifai kabisa, kwa sababu litapandisha gharama ya maisha. Ushuru uliopendekezwa kwa bidhaa zinazotoka ng’ambo kutaathiri wananchi kwa sababu bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini bado haziwezi kukimu mahitaji yetu; hivyo basi bado tutalazimika kuleta bidhaa kutoka ng’ambo. Kwanza tutengeneze viwanda vyetu kabla ya kuweka ushuru huu. Swali la fedha zitatoka wapi, basi wapunguze matumizi katika ofisi za serikali. Wametenga pesa nyingi kuhudumia wageni ili wapewe maji ya kunywa. Kama atakaa sana apewe githeri kama chakula chetu cha kitamaduni, sio kuwapa vyakula vya bei kama kuku kwa gharama ya wananchi. Mkate ni chakula cha kawaida kinachotumika katika kila asubuhi katika kila boma. Bei ya mkate ikipanda, basi tutakunywa chai na muguka . Serikali inapaswa kupunguza matumizi na safari za nje. Ikiwa ni lazima, Serikali inaweza tuma watu wasiozidi wawili kutuwakilisha. Sio kwenda watu thelathini na kuongeza ushuru ili kulipia safari hizi. Mikutano hii mnayohudhuria huko nje inaweza kufanywa katika boardroom zenu. Kwa hivyo, Mswada huu unapaswa kuangushwa kwa sababu wananchi wameusoma na kuukataa. Vijana wanaoandamana wamesoma Mswada huu katika mitandao, na wanajua kila The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}