GET /api/v0.1/hansard/entries/1441155/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1441155,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1441155/?format=api",
    "text_counter": 231,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Butere, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Nicholas Mwale",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana Mhe. Spika wa Muda kwa hii nafasi. Nimesimama kupinga Mswada huu wa Fedha mwaka wa 2024. Kama vile unajua, Wakenya wanahangaika, gharama ya maisha iko juu na Serikali ambayo iko kwa mamlaka ilitafuta kura na mamlaka ikiambia Wakenya kwamba watashukisha ushuru, wataweka pesa mfukoni, watabuni kazi na watafanya maisha yawe mema kwa ule Mkenya wa kawaida. Kwa hivyo, huu Mswada wa Fedha unaongeza ushuru ambayo ni kinyume na vile walieleza Wakenya. Huu Mswada unaongeza gharama kwa ubebaji wa miwa kutoka kwa shamba kuelekea kiwandani. Hiyo itadhuru bei ya mkulima kupata ile faida kutoka kwa miwa."
}